CRDB Bank Marathon Burundi yafikia lengo la kukusanya Faranga za Burundi Milioni 117 kusambaza tabasamu kwa wahanga wa maafa ya mafuriko Burundi.
Jeshi la Kusambaza Tabasamu (JLKT) kutoka Burundi katika mji wa Bujumbura siku ya leo limekamilisha misheni maalum ya CRDB Bank Marathon 2024 kwa kukusanya Faranga za Burundi Milioni 117 kwa ajili ya kuwasaidia wananchi waliopata maafa ya mafuriko Ziwa Tanganyika katika Mkoa wa Gatumba jijini Bujumbura.
Zaidi ya wanajeshi 1,500 ambao wamejitokeza kushiriki CRDB Bank Marathon Burundi, baada ya hapa, Jumapili ijayo, tarehe 18 Agosti 2024 Jeshi la Kusambaza Tabasamu litahitimisha misheni yake jijini Dar es Salaam kufurahi pamoja na Watanzania katika Viwanja vya The Green vilivyopo Oysterbay.
Karibu uungane na Jeshi la Kusambaza Tabasamu, 18 Agosti 2024, katika viwanja vya The Greens vilivyopo Oysterbay katika zoezi la kupitia njia tutakazozitumia tarehe 18 Agosti 2024, siku ya kilele cha CRDB Bank Marathon.
Kama bado haujajisajili, nafasi zimebaki chache na muda ni sasa. Unaweza kujisajili kupitia tovuti ya www.crdbbankmarathon.co.tz au tembelea kambi ya pale Mlimani City inayokuwa wazi kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa moja jioni kila siku.
PICHA ZA MATUKIO YA BURUNDI HIZI HAPA TAZAMA CHINI