Bondia wa Olimpiki Imane Khelif atafungua kesi ya unyanyasaji wa mtandaoni na ubaguzi wa rangi dhidi ya watu waliokuwa wakimtukana kuwa sio Mwanamke wakati wa mashindani ya Olympic nchini Ufaransa,
Imane Khelif kutoka Algeria alitwaa dhahabu katika kitengo cha uzani wa welterweight kwa wanawake Ijumaa ingawa alikosolewa sana kushiriki kama mwanamke sababu alifeli vipimo vya kudhibitisha ni mwanamke lililofanywa katika mashindano ya Chama cha Ndondi cha Kimataifa mwaka 2023.
Tambua Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa iliomba kutofautiana, nakusema Khelif alikidhi viwango vyote vya kushindana.