Kufuatia kuwepo na kushamiri kwa vitendo vya ukatili na ulawiti nchini, Umoja wa Wanawake wa Chama cha mapinduzi CCM Taifa (UWT) umepanga kuiomba serikali kubadilisha sheria ya wale wanaobainika kuwalawiti watoto wa kiume ili waweze kuhasiwa badala ya kufungwa maisha jela.
“Kwa mjibu wa kifungu cha sheria namba 154 (1) cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 kimetamka kuwa mtu yeyote ambaye anamuingilia mtu au mnyama kinyume na maumbile atakuwa ametenda kosa na atawajibika kwa adhabu ya kifungo cha maisha na wakati mwingine kifungo kisichopungua miaka thelathini (30)’.
Ni kauli ya Mwenyekiti wa UWT Taifa, Marry Chatanda, akizungumza katika uzinduzi wa dawati la kijinsia shule ya Sekondari ya Wavulana ya Bwiru.
Chatanda anasema, mbali ya Serikali kubadilisha sheria hiyo ili wanaume hao kuhasiwa pia amewashangaa wanaume hawaeleweki wanachohitaji na kuhoji wana shida gani kwa kuwa wanawake ni wengi kuliko wanaume na wengi hawajaolewa