Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), na John Pambalu, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana (BAVICHA), wamekamatwa na jeshi la polisi.
Tukio hili limetokea leo walipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Songwe, mkoani Mbeya, Tanzania.
Viongozi hawa walikuwa katika uwanja huo wa ndege kwa ajili ya kufuatilia sintofahamu inayoendelea, kufuatia kukamatwa kwa viongozi hapo jana August 11,2024 katika Ofisi za CHADEMA Kanda ya Nyasa akiwemo Makamu Mwenyekiti CHADEMA Bara Tundu Lissu, Katibu Mkuu John Mnyika na Mwenyekiti wa Kanda Joseph Mbilinyi (SUGU). ingawa maelezo zaidi bado hayajafahamika.
Taarifa zaidi zitatolewa kadri habari zitakavyopatikana.
#KonceptTvUpdates