Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Dkt. Mathayo Mathayo, amepongeza hatua kubwa ya maendeleo ya ujenzi wa jengo la Wizara ya Madini, ambalo kwa sasa limefikia asilimia 84.4. Akiwa jijini Dodoma leo Agosti 12, 2025, Dkt. Mathayo alipokea taarifa ya maendeleo hayo na kupongeza juhudi zinazofanyika.
Ujenzi wa jengo hilo la ghorofa tano unatarajiwa kukamilika licha ya changamoto mbalimbali zilizojitokeza, ikiwemo kuchelewa kwa vifaa kutokana na upungufu wa fedha za kigeni. Serikali inajitahidi kuhakikisha changamoto hizo zinapatiwa ufumbuzi ili kufanikisha kukamilika kwa ujenzi huo kwa asilimia zilizobakia.
Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, alisisitiza kuwa mkandarasi atahakikisha jengo linakamilika kwa wakati, ingawa changamoto kadhaa ziliathiri ratiba ya awali ya kukamilisha ujenzi huo.
Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Katibu Mkuu, Mhandisi Yahya Samamba, Naibu Katibu Mkuu Msafiri Mbibo, pamoja na maafisa wengine wa wizara.
#KonceptTvUpdates