Kesi inayowakabili Paul McKenzie, kiongozi wa kanisa la kufunga hadi kufa, na washukiwa wengine 94 imeibua mjadala mkali juu ya mipaka ya uhuru wa kuabudu na jukumu la serikali kulinda maisha ya raia wake. McKenzie na wenzake walisimama kizimbani mjini Mombasa leo, wakikanusha mashtaka ya kuua bila kukusudia kufuatia vifo vya waumini zaidi ya 400 katika Msitu wa Shakahola, pwani ya Kenya.
McKenzie, ambaye alikamatwa Aprili mwaka huu, anadaiwa kuwashawishi wafuasi wake kufunga hadi kufa ili “kumlaki Yesu.” Tukio hili limeshtua taifa na kuleta mshtuko duniani kote, huku likitoa changamoto kwa mamlaka juu ya jinsi ya kushughulikia makundi yenye imani kali.
Wakati kesi hii ikiendelea, maswali yanaibuka juu ya jukumu la serikali katika kudhibiti makundi ya kidini ambayo yanaweza kuhatarisha maisha ya wafuasi wake. Je, serikali ilipaswa kuchukua hatua mapema kuzuia msiba huu? Na kwa kiasi gani uhuru wa kuabudu unaweza kuingiliwa kwa lengo la kulinda maisha ya watu?
Mwendesha mashtaka Alexander Jami Yamina alielezea kuwa kesi hii ni ya kipekee nchini Kenya, na washukiwa wanakabiliwa na mashtaka chini ya sheria inayohusiana na makubaliano ya kujitoa uhai. Serikali imejitayarisha vyema, ikikusanya mashahidi 420 ili kuthibitisha kesi yao dhidi ya McKenzie na wenzake.
Mwishoni mwa mwezi Machi, mamlaka ilianza kurudisha miili ya waathiriwa kwa familia zao, baada ya kazi ngumu ya kuwatambua kwa kutumia teknolojia ya DNA. Hadi sasa, miili 34 imerejeshwa kwa ndugu zao.
Kesi hii inatarajiwa kuendelea kwa siku nne, na itakuwa ya kipekee si tu kwa sababu ya idadi kubwa ya waathiriwa, bali pia kwa sababu ya masuala nyeti inayoyainua kuhusu imani, uhuru wa kuabudu, na wajibu wa serikali katika kulinda maisha ya watu wake.
Licha ya kiongozo huyo (Paul McKenzie), kukana mashtaka ya mauaji ya kutokusudia kufuatia vifo vya waumini zaidi ya 400 katika mkasa unaohusiana na ibada katika pwani ya Kenya.
McKenzie, ambaye alianzisha Kanisa la Good News International Church mwaka wa 2003, alidai kuwa alilifunga mwaka wa 2019 na kuhamia Shakahola kujiandaa kwa kile alichotabiri kuwa mwisho wa dunia Agosti mwaka jana. Matukio haya yanaacha alama kubwa katika jamii na yanawafanya Wakenya na dunia kwa ujumla kufikiria upya kuhusu usalama wa wafuasi katika mazingira ya kiimani.
#KonceptTvUpdates