Mwanamuziki aliyekuwa anaunda kundi la PSQUARE, Peter Psquare kwa mara ya kwanza amefunguka toka kundi hilo kuripotiwa kuvunjika na kusema ndugu yake ameamua kugeuza kundi lenye Tuzo nyingi kuwa kichekesho.
Kama utakumbuka wiki iliyopita taarifa ya kundi La P-Square kuvunjika kwa mara ya 3, ilithibitishwa na Rude Boy wakati akiwa kwenye Interview na City FM huko Nigeria.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Peter ameweka barua ya wazi kwenda kwa Pacha wake ambae walikuwa wanaunda kundi hilo Paul Okoye (Rude Boy) aonesha jinsi ameumia na maneno ya kibinafsi ambayo amekuwa akiyaongea Rude Boy kwenye mahojiano mbalimbali.
Ambapo kwenye barua hiyo amesema ndugu yake huyo amegeuza kundi lenye Tuzo nyingi kuwa kichekesho na kutolea ufafanuzi juu ya kauli za Rude Boy kujisifu kuwa yeye ndiye ambae amekuvwa akihusika kwa asilimia 99 kwenye kazi za PSquare kwa kuandika na kuimba akidharau nguvu alizotumia kwenye Projects zao.
Mbali na hilo Peter amesema pacha wake amekuwa akifanya Kila kitu Mashabiki wamchukie lakini haijawahi hivyo kwa sababu kama ni kuchukiwa watachukiwa wote kwa kuwaangusha mashabiki wa muziki wao.