Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro ameagiza kusitishwa kwa ujenzi wa shule ya msingi katika eneo la michezo lililopo mtaa wa Panga, Tegeta Wazo Jijjini Dar es Salaam.
Ndumbaro amefikia uamuzi huo kufuatia pingamizi la wananchi kukataa ujenzi wa shule hiyo katika eneo ambalo limekua likitumika kwa shughuli za michezo.
Hata hivyo, Waziri Ndumbaro amewataka viongozi wa kata hiyo na wananchi kutafuta eneo lingine ambalo litatumika katika ujenzi wa shule hiyo ambapo pia ametoa siku tatu kwa mkandarasi na viongozi wa Halmashauri kurudisha uwanja katika hali yake ya kawaida ili uanze kutumika.