Wachezazji sita kutoka ligi kuu ya England, Bukayo Saka, Cole Palmer, Kobbie Mainoo, Alejandro Garnacho, Joao Pedro na Michael Olise wameteuliwa kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora Chipukizi wa Mwaka, PFA kwa msimu wa 2023/24.
Nyota wa Arsenal, Bukayo Saka yuko katika kinyang’anyiro cha kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora Chipukizi mfululizo baada ya kushinda tuzo hiyo mwaka jana, mwaka huu anatarajia ushindani mkali kutoka kwa Waiingereza wenzake akiwemo Cole Palmer anayeiwakilisha Chelsea, na Kobbie Mainoo wa Manchester United.
Wengine walioteuliwa kuwania tuzo hiyo ni pamoja na nyota wa Brighton and Hove Albion Joao Pedro na Alejandro Garnacho wa Manchester United na pia kiungo Michael Olise ambaye ameondoka Crystal Palace kwenda Ujerumani kujiunga na klabu ya Bayern Munich.
Mshindi atatangazwa rasmi katika hafla ya tuzo hizo za PFA mjini Manchester, Jumanne ijayo, Agosti 20, 2024.