William Masvinu, raia wa Zimbabwe amejizoelea umaarufu kwa kushinda shindano la ‘Mtu Mwenye Sura Mbaya Zaidi’ aka Mr Sura Mbaya nchini humo, akiweka rekodi ya kutwaa taji hilo kwa mara tano mfululizo.
Ushindi wake umempa umaarufu wa ndani na nje ya Zimbabwe, huku shindano hilo likivutia macho na masikio ya wengi.
Muandaaji wa mashindano hayo David Machowa alisema, anataka watu wenye sura mbaya ‘wabaya’ wapate fursa sawa mashindano kama ya urembo ama warembo.
Mshindi wa shindano hilo amepokea zaidi ya kiasi cha Shilingi Milioni Moja na Laki tatu na ng’ombe.
Mara kadhaa, Masvinu amenukuliwa akisema kuwa anajisikia fahari na sura yake akitaka mashindano ya aina hiyo yapewe hadhi ya kimataifa.
Picha kadhaa za William Masvinu zimekuwa zikitumika kwenye utani katika mitandao ya Jamii zikitengenezewa kama ‘Stika’ zinazo tumika katika mtandao wa WhatsApp na mingineyo.
#KonceptTvUpdates