Klabu ya Al Nassr imefanikiwa kutinga Fainali ya Saudi Super Cup 2024 baada ya kuifunga Al Taawoun mabao 2-0 katika mchezo wa Nusu Fainali uliopigwa uwanja wa Prince Sultan bin Abdulaziz.
Mabao ya Al Nassr yamefungwa na kiungo raia wa Saudi Arabia, Ayman Yahya dakia ya 8′ na mshambuliaji wa Ureno, Cristiano Ronaldo dakika ya 57′.
Rasmi Al Nassr watacheza Fainali na klabu ya Al Hilal siku ya Jumamosi, Agosti 17 katika uwanja huo huo wa Prince Sultan bin Abdulaziz.
Al Hilal wametinga Fainali baada ya kupata ushindi wa mikwaju ya penati 4-1 baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya kufungana 1-1.
Fainali ya mwisho ya Saudi Super Cup ambapo timu hizo zilikutana ilikuwa Januari 30, 2021 na klabu ya Al Nassr ilibuka na ushindi wa mabao 3-0.