Klabu ya KMC FC imetangaza kumrudisha nyumbani Kiungo wake,Awesu Ally Awesu ambaye siku kadhaa nyuma alitambulishwa kama Mchezaji wa Simba.
Awesu anarejea KMC baada ya kushindwa kesi TFF ambayo timu yake ilimshitaki kuvunja mkataba kutokufuata utaratibu na kutimukia katika klabu ya Simba.
Bodi ya Ligi na haki za wachezaji baada kujiridhisha pande zote mbili kati ya mchezaji na KMC, kutambua kuwa Awesu Awesu bado wanamtambua kuwa mchezaji wa KMC na bado ana mkataba wa mwaka mmoja na timu yake na kumwammbia arejee kwenye timu yake kutumikia mkataba wake.