Mahakama ya Wilaya ya Bagamoyo imemuhukumu Gudulo Suma Manyama (54) Mkulima mkazi wa Mzuki zuki- Kiwangwa Bagamoyo kwenda jela miaka 30 kwa kumbaka binti wa miaka 14.
Mtuhumiwa amekuwa akifanya kitendo hicho kwa nyakati tofauti tofauti kuanzia 2023 hadi Mei 2024 ilipobainika katika Kijiji Cha Mzukizuki Kiwangwa, wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani.
Hukumu hiyo imetolewa mahakamani hapo ambapo mtuhumiwa alifanya mapenzi na binti yake mlezi kinyume na Sheria na kupelekea adhabu hiyo
Akisoma hukumu hiyo mahakamani hapo mh Mmanya SRM tarehe 12.08.2024 alisema baada ya ushahidi kukamilika mtuhumiwa ametiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa hilo la kufanya mapenzi na binti wa miaka 14.