Real Madrid imetwaa kombe la UEFA Super Cup kwa mara ya sita kufuatia ushindi wa 2-0 dhidi ya Mabingwa watetezi wa Europa League, Atalanta.
Magoli ya Real Madrid katika mchezo huo uliopigwa katika dimba la PGE Narodowy mjini Warsaw, Poland yamefungwa na Federico Valverde dakika ya 59′ na nyota mshambuliaji mpya wa klabu hiyo Kylian Mbappe dakika ya 68′.
Kylian Mbappé amefunga bao lake la kwanza ndani ya uzi wa Real Madrid akiifungia Real Madrid bao la pili na la ushindi katika mchezo huo.
Huku kocha Carlo Ancelotti akiweka rekodi ya kuwa kocha aliyetwaa mataji mengi zaidi ya UEFA Super Cup, akitwaa taji ilo mara 5.
Akiwa katika na klabu ya AC Milan mwaka 2003 na 2007 pamoja na Real Madrid mwaka 2014, 2022 na mwaka huu 2024.
Kocha anayefatia kwa kutwaa taji ilo mara nyingi ni Pep Guardiola akitwaa mara nne akiwa na Barcelona mwaka 2009 na 2011, Bayern München mwaka 2013 na Man City mwaka 2023.
Wachezaji Dani Carvajal na Luka Modrić ndio wachezaji walio na mataji mengi zaidi ya UEFA Super Cup kila mmoja akishinda mara tano Real Madrid ndiyo klabu iliyo na mataji mengi zaidi ya UEFA Super Cup wakitwaa taji ilo mara sita, wakifatiwa na AC Milan na Barcelona walioshinda mara tano kila mmoja.
Imeandikwa na Shabani Rapwi