Mwanasheria wa klabu ya Yanga, Simon Patrick kupitia ukurasa wake wa instagram amendika ujumbe huu kuhusu sakata la mchezaji Awesu Awesu “Kuhusu suala la Awesu, kwanza napenda kuipongeza Kamati ya Sheria kwa kutoa uamuzi wa haki, Bravo!.
Lakini kwa maslahi ya soka letu, Kamati ilipaswa kwenda mbali na kulitazama suala hili kwa mtazamo wa kisheria kwa mujibu wa (RSTP) badala ya kuangalia malalamiko ya KMC pekee:
1. Kuvunja Mkataba bila sababu za kisheria: kitendo cha mchezaji kurudisha fedha na kujiunga na timu nyingine ni ushahidi wa wazi kuwa mchezaji alivunja mkataba, na adhabu yake imeelezwa kwenye sheria.
2. Kushawishiwa na watu wa nje (third-party influence): kitendo cha mchezaji aliyetoroka na kutambulishwa na timu nyingine wakati bado ana mkataba halali na timu yake, hakihitaji ushahidi wa ziada kuthibitisha ushawishi huo, na adhabu yake imeelezwa kwenye sheria.
Kutoiadhibu klabu iliyomtambulisha mchezaji mwenye mkataba ni kufungua mlango mwingine mbaya sana kwenye soka letu, na hakuna atakayeweza kuufunga kwa sababu itakua “double standard” emphasis added.
Haya ni maoni yangu binafsi! NB: Ifike mahali watanzania tukubaliane kati ya busara na sheria nini tufate.”.