Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri, amesema Wizara ya Maji imeandaa mafunzo ya siku mbili katika kuhakikisha usalama wa mabwawa ya maji na tope sumu unaimarishwa.
Amesema mafunzo hayo yameandaliwa kwa kushirikiana na Tanzania Chamber of Mines na yatafanyika mkoani Mwanza .
Amesema hayo katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Maji uliopo Mtumba Jijini Dodoma.
Ameongeza kuwa mafunzo yatahusisha watalaam kutoka wamiliki wa migodi kwa ajili ya usalama wa mabwawa ya tope sumu, wamiliki wa mabwawa makubwa ya maji, wataalam wa mabwawa waliosajiliwa na wataalam kutoka Serikalini.
Wizara ya Maji kupitia Idara ya Rasilimali za Maji ina jukumu la kuhakikisha mabwawa ya maji na tope sumu yanakidhi vigezo vya usalama wa mabwawa kwa mujibu wa Sheria ya Rasilimali za Maji Na. 11 ya Mwaka 2009 na maboresho yake Na. 8 ya Mwaka 2022. Pamoja na kanuni za usalama wa mabwawa GN 237 za mwaka 2013 na mabresho yake GN 55 ya mwaka 2020.
#KonceptTvUpdates