Msanii wa vichekesho vya kuigiza sauti na kuingiza sauti kwenye video mbalimbali, ambaye anajulikana kwa jina la @mkalimani_og, amefunguka kuhusu changamoto zake za kifedha katika kipindi cha #Pilikapilika. Akiwa na uzoefu wa miaka minne tangu alipoanza kazi hiyo mwaka 2020, msanii huyo ameeleza kuwa anatumia kiasi cha shilingi elfu ishirini (20,000) kwa siku kwa ajili ya bando la data.
Katika maelezo yake, msanii huyo amesema kwamba licha ya matumizi haya makubwa ya fedha kwa bando, hadi sasa hajafanikiwa kurudisha pesa alizotumia katika kipindi hicho. Hali hii imekuwa changamoto kubwa kwa msanii huyo, akieleza kuwa licha ya kujitahidi kuboresha kazi yake na kujituma katika tasnia ya vichekesho, changamoto za kifedha zinaendelea kuwa kikwazo.
Msanii huyo ametoa mwito kwa wadau na wapenzi wa vichekesho kutambua juhudi zinazofanywa na wasanii katika kuleta burudani, na kuwaunga mkono ili kuboresha hali yao ya kifedha na kuendelea kutoa kazi bora.
#KonceptTvUpdates
#EastAfricaRadio