Klabu ya Namungo FC, maarufu kama “Wauaji wa Kusini,” leo Ijumaa tarehe 16 Agosti 2024, saa 8 mchana, watazindua jezi zao mpya za msimu wa 2024/2025. Jezi hizi mpya zinajivunia ubora wa hali ya juu, zikiakisi kila sifa inayostahili kuitwa jezi bora.
Uzinduzi huo utashuhudia utolewaji wa aina mbalimbali za jezi, ikiwemo jezi za nyumbani (HOME), za ugenini (AWAY), pamoja na jezi za mazoezi na kwa timu ya wafanyakazi (Staff). Kila jezi imeundwa kwa kuzingatia ubunifu na ubora, ikiwakilisha kikamilifu utambulisho wa klabu na kuleta mwonekano wa kisasa na wa kuvutia.
Mashabiki na wapenzi wa soka nchini wanatarajia kuona jezi hizi mpya zikiwapa nguvu na morali wachezaji wa Namungo FC wanapokabiliana na changamoto za msimu mpya. Uzinduzi huu ni ishara ya maandalizi makubwa ya timu kuelekea msimu mpya, huku wakilenga kufanya vizuri zaidi na kuleta ushindani mkali kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara.
#KonceptTvUpdates