Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) imeujulisha umma wa Watanzania kuhusu mabadiliko ya ratiba ya mapokezi ya ndege yake mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner nchini Tanzania.
Taarifa ya ATCL ya leo Agosti 19, 2024 imebainisha kuwa mabadiliko hayo yamesababishwa na changamoto ya hali ya hewa ambayo iko nje ya uwezo wao hivyo kupelekea kubadilisha ratiba ya safari.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa ratiba mpya ya kuwasili kwa ndege hiyo itatolewa huku Kampuni hiyo ikiomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.