Msanii wa muziki wa Bongofleva Rajab Abdul alimaarufu kama Harmonize atakiwa kuilipa Benki ya CRDB fidia ya Millioni 10, gharama za kesi na Deni la Mkopo la Tsh. Milioni 103 baada ya kushindwa kulipa kikamilifu Mkopo wa Tsh. Milioni 300 tokea Mwaka 2019.
CRDB na Harmonize walikubaliana angefungua akaunti ya Kibiashara katika benki hiyo kisha kuweka Tsh. Milioni 100 na kuifanya akaunti hiyo kuwa akaunti yake kuu katika shughuli zake za Kibiashara, lakini alikiuka makubaliano hayo.
Benki ya CRDB ilifikia uamuzi wa kwenda Mahakamani baada ya usumbufu wa ulipaji deni kutoka kwa msanii
huyo, ambapo Mahakama ilitoa wito mara kadhaa kwa Msanii huyo lakini hakufika Mahakamani.
Harmonize anatakiwa kuilipa Benki hiyo kiasi cha milioni 103 kutokana na mkopo aliyouchukua katika benki hiyo na kushindwa kulipa kwa kuzingatia makubaliano yaliyowekeana na Benki hiyo.
Credit : Jamii Forums..