Miongoni mwa taarifa kutoka jimbo la Niger zinasema kuwa majambazi wengi sasa wamejifanya wakazi wa mji wa Allawa, wakiishi katika nyumba za wakazi waliokimbia na kulima mashamba yao kwa kutumia mbolea iliyobaki kwenye nyumba hizo.
Majambazi hao walivamia mji wa Allawa miezi mitano iliyopita, na tangu wakati huo, wamewalazimisha wakazi wa mji huo kukimbia na kuwa wakimbizi. Mkazi mmoja wa Allawa ambaye yuko uhamishoni ameiambia BBC kwamba tukio hilo lilitokea baada ya serikali kuondoa vikosi vya usalama vilivyokuwa vikilinda mji huo, ikidai kuwa ilikuwa inabadili mfumo wa ulinzi. Hata hivyo, wanajeshi hawajarudishwa hadi sasa.
“Baadhi yetu tulijaribu kurejea mjini kwa matumaini kuwa hali imetulia, lakini tulikuta nyumba zetu zimechukuliwa na majambazi, ambao wanatumia hata mbolea tuliyoiacha. Sasa wanamiliki na kulima mashamba yetu katika msitu wa Allawa,” alisema mkazi huyo kwa masikitiko.
Hali hii imezua hofu kubwa miongoni mwa wakazi waliokimbia, huku wakihofia usalama wao na matumaini ya kurejea kwenye makazi yao yakiendelea kupungua. Serikali bado haijatoa tamko rasmi kuhusu kurejesha vikosi vya usalama ili kukabiliana na hali hiyo.
#KonceptTvUpdates