Mbunge wa Jimbo la Tanga Mhe Ummy Mwalimu amewataka wananchi wake kuendelea kutumia Michezo kuhamasisha umoja, Mshikamano na amani pamoja na kueleza kazi kubwa na nzuri zinazofanywa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ndani ya Jiji la Tanga na Tanzania.
Ummy ameyasema hayo kwenye Fainali ya Mabawa Super Cup iliyozikutanisha timu ya Duga Fc dhidi ya Mwanzange Fc, mchezo uliochezwa katika shue ya msingi Mikanjuni Jijini Tanga, ambapo mshindi hakuweza kupatikana kutokana na mchezo kuvunjika.
Akizungumza na wananchi hao Ummy amesema wana Tanga wana kila sababu ya kumuunga mkono Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kutokana na Miradi mikubwa ya Kimkakati inayotekelezwa katika Jiji la Tanga ikiwemo Elimu, Maji, barabara pamoja na maboresho ya bandari ya Tanga iliyoanza kupokea Meli kubwa za mizigo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mabawa Super Cup, Athumani Sheria amesema lengo la kuanzisha mashindano hayo ni kwa ajili ya kupambana na Changamoto mbalimbali zinazowakabili vijana na jamii ikiwemo kusaka vipaji, kupinga ukatili na unyanyasaji wa kijinsia, matumizi ya madawa ya kulevya, maambuzi ya VVU pamoja na kuunganisha vijana.