atuhumiwa wanne wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma kufuatia video iliyosambaa katika mitandao ya kijamii ikionesha binti akiingiliwa kinyume na maumbile na kikundi cha watu huku wakidai wametumwa na afande kufanya uovu huo.
Akizungumza leo Jijini Dodoma mara baada ya kusomwa kwa mashtaka yanayowakabili washtakiwa hao, Mkurugenzi Msaidizi wa Makosa dhidi ya Binadamu kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Renatus Mkude amesema wanne hao wanashtakiwa kwa makosa mawili ambayo ni kumwingilia kinyume na maumbile msichana huyo na kumbaka kwa kundi (gang rape).
Amesema kuwa kesi hiyo itaendelea kusikilizwa kwa siku tano mfululizo hadi Ijumaa na kwamba haki itatendeka kwa watakaopatikana na hatia.