Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetangaza kuwa ndege mpya ya Air Tanzania aina ya Boeing B787-8 Dreamliner, ambayo ilikumbwa na changamoto za hali ya hewa na kushindwa kuondoka Marekani kwa wakati uliopangwa, itawasili leo. Ndege hiyo inatarajiwa kutua majira ya saa 10 jioni katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume.
Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi, atakuwepo uwanjani kupokea ndege hiyo, ambayo inatarajiwa kuongeza uwezo wa shirika hilo la ndege katika kuhudumia safari za kimataifa. Ujio wa ndege hii mpya ni sehemu ya mpango wa serikali wa kuboresha na kuimarisha sekta ya usafiri wa anga nchini.
Ndege hiyo ni miongoni mwa ndege za kisasa zaidi duniani, ikiwa na uwezo wa kubeba abiria wengi huku ikitumia mafuta kwa ufanisi zaidi, jambo linaloweka Tanzania katika nafasi nzuri ya ushindani kwenye soko la kimataifa la usafiri wa anga.
#KonceptTvUpdates