Watu wanne wamefariki dunia na wengine kujeruhiwa hii leo Agosti 22, 2024, kwenye ajali iliyohusisha lori la mafuta na basi la Baraka lililokuwa likitokea Dodoma kuelekea Dar es Salam, katika eneo la Vigwaza Chalinze mkoani Pwani.
Akithibitisha kuwepo kwa ajali hiyo Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, amesema ajali hiyo imesababisha vifo vya watu wanne ambao wote ni wanawake pamoja na mtoto mdogo ambaye umri wake haujafahamika.