Waziri wa Maji Jumaa Aweso (Mb) amewasilisha taarifa ya hali ya upotevu wa maji (Non Revenue Water) kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira.
Aweso amesema Wizara ya Maji kupitia Chuo Cha Maji imebuni na kufanikisha teknolojia ya kisasa kwa ajili kutambua maeneo ambayo yanaupotevu wa maji katika miundombinu ya maji ili kuwezesha utatuzi wa haraka wa changamoto hiyo.
Amesema teknolojia hiyo imeanza kutumika kwenye baadhi ya maeneo na imeonesha ufanisi mkubwa hivyo Wizara inaendelea na jitihada kuhakikisha teknolojia hiyo inatumiwa na taasisi zote za sekta ya maji ambazo zinatoa huduma ya maji kwa wananchi.
Kamati ya Kudumu ya Bunge kupitia kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Jackson Kiswaga (Mb) wameipongeza Wizara kwa ubunifu huo na kuwataka kuhakikisha ubunifu huo unasimamiwa ili kuleta tija kwa jamii
#KomceptTvUpdates