Maria Branyas Morera, Mhispania mzaliwa wa Marekani anayeaminika kuwa mtu mzee zaidi duniani amefariki dunia.
Maria aliyetajwa kuwa mtu mzee zaidi aliye hai duniani katika kitabu cha Rekodi za Dunia cha Guinness Januari 2023 alifariki dunia Agosti 19, 2024 akiwa na umri wa miaka 117 siku 168.
Imeelezwa kuwa, Maria aliyezaliwa Mwaka 1907 aliaga dunia kwa amani katika Makazi ya Kulea wazee huko Catalonia, Uhispania, ambako aliishi kwa miongo miwili iliyopita.