Ameandika Farhan Kihamu, Mchambuzi wa Soka wa Clouds FM
Tunaweza tusikubaliane hapa ila naamini Ligi ya Zambia kwasasa sio sehemu sahihi ya timu za Tanzania kuchukua Wachezaji, Ligi ya Malawi sio sehemu sahihi, Ligi ya Rwanda sijui Burundi sio sehemu sahihi, Ligi sijui za Cameroon mara Nigeria ama Ghana napo sio kweli sio sehemu sahihi ya kuchukua Wachezaji, Ligi ya Ivory Coast kwa mbaali panafaa kiasi chake.
Ni kwanini? Ni kwasababu ligi nyingi nilizotaja hapo zipo chini yetu, Ligi yetu ipo SITA BORA Afrika, automatically Mchezaji akifunga mabao 30 huko Cameroon ama Burundi ni sawa na mabao 10 kwenye Ligi yetu, kwa hoja ya uwekezaji wetu, ushindani wetu na ubora wetu, kadri muda unavyozidi kwenda ligi za nchi hizo zitakuwa na quality ya Wachezaji wa timu zao kucheza Championship hapa kwetu, kifupi ubora usiachane sana.
Wenzetu Ligi nyingi kuna vifungu wanaweka mfano EPL Mchezaji acheze kutoka Taifa ambalo linarank nafasi za 70+ kwenye viwango vya FIFA with exception ndogo sana kwa baadhi ya Wachezaji ambapo wanatazama pia Ligi aliyotoka, lazima kuwe na namna ya kulinda quality ya Ligi kuepusha gharama kwa timu zetu.
Tags: MICHEZO