Mfanyabiashara na Mfugaji maarufu wa Nguruwe Jijini Dodoma, Dr. Manguruwe amesema anapanga kumpelekea ofa nono mwanachama wa Yanga, Haji Manara ya Tsh Milioni 10 kwa mwezi awe Msemaji wake.
Dr Manguruwe ametoa kauli hiyo baada ya Rais wa Yanga, Hersi Said kusema kuwa Manara kwa sasa sio msemaji wa Yanga badala yake wanamtafutia sehemu nyingine ya kumpa kazi ndani ya klabu hiyo.
Ameongeza kuwa Yanga imemvunjia heshima ambayo ameijenga kwa muda mrefu na gharama kubwa Msemaji huyo nguli wa Soka, hivyo anataka awaoneshe ukubwa wa Haji kwa kumpa mshahara mkubwa.