Mwimbaji wa Bongo Fleva, Zuchu ameahidi kumpatia zawadi ya Gari aina ya Crown Msanii Anjella lenye thamani ya Milion 15.
Hii ni baada ya Anjella kuchelewa kwenye Interview katika kipindi cha Lavidavi kinachorushwa na kituo cha Wasafi FM.
Mtangazaji wa kipindi hiko Diva TheeBawse alimuomba msanii Zuchu na mpenzi wake Diamond Platnmz kumnunulia gari Angella na kumkubalia.
Anjella hakuamini macho yake na kujikuta akitokwa na Machozi ya furaha baada ya kusikia atapatia zawadi hiyo, Gari lake atakabidhiwa siku ya kesho makao makuu ya kituo hicho.