Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko, ameshiriki kongamano la Nishati Safi ya Kupikia linalofanyika katika Hoteli ya Kwanza, Kizimkazi-Zanzibar, leo tarehe 23 Agosti 2024. Kongamano hili lina lengo la kuhamasisha matumizi ya nishati safi na teknolojia zinazohusiana.
Kabla ya kongamano, Dkt. Biteko alitembelea mabanda ya maonesho ya wadau wa sekta ya nishati safi ya kupikia, ambapo alijifunza kuhusu teknolojia mpya na elimu inayotolewa kuhusu matumizi salama ya nishati hiyo. Kaulimbiu ya kongamano hilo, “Upishi Salama kwa Afya ya Mpishi na kwa Maendeleo ya Jamii,” ina lengo la kuongeza ufahamu kuhusu faida za nishati safi kwa afya ya mpishi na maendeleo ya jamii kwa ujumla.
#KonceptTvUpdates