Msani Edrisah Kenzo Musuuza maarufu kwa jina la Eddy Kenzo ameteuliwa kuwa Mshauri wa Rais Yoweri Museveni katika masuala ya Sanaa.
Kuteuliwa kwa Eddy Kenzo kumetangazwa na mke wake katika mtandao wa kijamii wa X zamani twitter.
Edrisah Kenzo ameteuliwa katika nafasi hiyo ambapo alikuwa Mwenyekiti wa Shirikisho la Wasanii nchini Uganda lakini pia akiwa swahiba sana wa Rais wa Uganda.
Itakumbukwa kuwa mke wa Eddy Kenzo,Phiona Nyamutoro ni Katibu Mkuu katika wizara ya madini nchini Uganda.