Mradi wa Uwanja wa Suluhu, unaotarajiwa kuwa kituo kikuu cha michezo na shughuli za kijamii, umeanza rasmi na awamu ya kwanza itajikita katika ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu. Akizungumza kuhusu mradi huo, Mhandisi Vay Robert Matunda, mkandarasi wa mradi, alisema kwamba hatua hii itazingatia ujenzi wa uwanja wenye uwezo wa kubeba watu 20,000, ambapo utahusisha shughuli za mpira wa miguu pekee.
Mhandisi Matunda alifafanua kwamba mradi huu utakuwa na huduma mbalimbali zinazozunguka uwanja, ikiwa ni pamoja na hosteli, vyoo, na kumbi za mikutano, ambazo zitasaidia katika kutoa mazingira mazuri na fursa kwa watu wa maeneo ya Makunduchi na Kizimkazi.
“Kutakuwa na huduma mbalimbali kuzunguka uwanja kama hosteli na vyoo, kumbi za mikutano ni miongoni mwa vitu vitakavyouzunguka uwanja ili kusaidia kuwa na mazingira mazuri na kutoa fursa kwa watu wa maeneo ya Makunduchi na Kizimkazi. Pia, uwanja huu utakuwa na uwezo wa kubeba watu elfu ishirini,” alisema Matunda.
#KonceptTvpdates