Wizara ya Afya ya Kenya imethibitisha kesi ya pili nchini humo ya Ugonjwa hatari wa Mpox ambao zamani ulijulikana kama homa ya Nyani.
Wagonjwa wote wawili wametajwa kuwa ni Wanaume, Madereva wa Malori waliotokea Congo DRC.
Hivi karibuni, kituo cha kuzuia na kudhibiti magonjwa barani Afrika (CDC), kiliutangaza mlipuko wa Mpox kuwa ni dharura ya afya na usalama wa umma barani Afrika.