Waziri wa Fedha na mwanachama wa Yanga SC Mwigulu Nchemba amesema kuwa anajua sakata lote la mchezaji wa zamani wa Singida Fountain Gate Yusuph Kagoma ambaye kwa sasa ni mchezaji wa Simba SC.
Ameongezea kwa kusema kuwa, mcgezaji huyo alisaini mkataba na Yanga SC na ilo analijua ila amewaomba Yanga waondoe shauri ilo ili mchezaji aweze kucheza.
“Nafahamu undani wa Suala la Yusuf Kagoma, ni kweli Kagoma alisaini mkataba Yanga, na baadae akasaini Simba, Najua kutokwenda kwake Yanga na badala yake kusaini Simba hata sio Masuala ya Fedha. Tutatumia muda sana tukitaka kuchimba haya. Kagoma ni mtoto wetu.
Yanga ni Club kubwa sana na ina mambo muhimu ya kuyawekea nguvu kuyafanikisha kuliko kuweka nguvu Kagoma aisicheze licha ya ukweli kwamba alistahili achezee Yanga.
“Nimewaomba viongozi wa Yanga SC wamsamehe Kagoma na yote, waondoe shauri dhidi ya Kagoma, wamwachie awe huru akaitumikie Simba SC kwa maslahi mapana ya mpira wa Tanzania na kwa faida ya mchezaji mwenyewe.” Amesema Mwigulu Mwanachama Yanga SC.