Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Samia Suluhu Hassan amesema atasimamia shabaha ya kuwa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) madhubuti na lenye maofisa na askari wenye weledi, ari na zana bora.
Aliyasema hayo wakati akifunga zoezi la Medani katika kuadhimisha Miaka 60 ya JWTZ katika eneo la Pongwe Msungura, lililoko Msata.
Rais Samia alisisitiza kuwa jeshi imara zaidi litatokana na dhamira ya kweli, moyo wa kujituma na uchumi imara zaidi.
Vilevile, Amiri Jeshi Mkuu aliitaka JWTZ kuendelea kulinda misingi ya kuanzishwa kwa jeshi hilo na kuendelea kudumisha nidhamu, utii, uaminifu na uhodari uliopo katika jeshi hilo.