Mamlaka ya Rwanda ilitangaza Alhamisi kupiga marufuku shughuli za Madhehebu 43 ya Kidini kote nchini kuanzia Agosti 28, wiki chache baada ya kufungwa kwa Maelfu ya Makanisa.
Barua iliyotolewa na Wizara ya Tawala za Mitaa inawataka viongozi wa Wilaya kutekeleza marufuku hiyo, ikisema tathmini inayoendelea ilibaini kuwa mashirika ya kidini yanafanya kazi kinyume na kanuni zilizopo.
Makundi mengi yaliyoathiriwa yalikuwa ya madhehebu ya Kipentekoste, likiwemo Kanisa la Kilutheri, Mwanachama wa Shirikisho la Kilutheri la Ulimwengu lililoanzishwa miaka ya 1990 nchini Rwanda ili kuendeleza kazi ya Wamishonari wa Ujerumani.
Hatua hiyo imekuja wiki kadhaa baada ya Mamlaka kufunga Makanisa 5000 yanayoshutumiwa kwa kushindwa kufikia viwango vinavyohitajika kisheria na kuweka maisha ya waabudu katika hatari zisizo za lazima.
Mamlaka ilisema asilimia 59.3 ya Makanisa 13,000 yaliyokaguliwa mwishoni mwa Julai yalikuwa yamefungwa kwa sababu ya kutofuata sheria.