Somalia imetishia kusitisha safari zote za Ndege za Ethiopian Airlines kuelekea katika ardhi yake kutokana na mzozo unaoendelea.
Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Somalia (SCAA) ilitangaza mnamo Agosti 21, 2024, kwamba Shirika la Ndege limeshindwa kujibu masuala yanayohusiana na uhuru wa Somalia.
Mzozo huo uliongezeka baada ya Ethiopia kutia saini makubaliano mnamo Januari 2024 na eneo linalojitenga la Somaliland, kupata ufikiaji wa kilomita 20 za ukanda wa pwani wa Somaliland kwa miaka 50 kwa kubadilishana na kulitambua eneo hilo.
Somalia inauona mkataba huu kama ukiukaji wa moja kwa moja wa Mamlaka yake, na hivyo kuzidisha mvutano kati ya nchi hizo mbili.
Shirika la ndege la Ethiopia linatakiwa kushughulikia masuala haya, la sivyo safari zote za Ndege kuelekea Somalia zitasitishwa.