Chama cha ACT Wazalendo kimesema hivi karibuni kumeibuka tena kwa kasi matukio ya utekaji, kupotea na mauaji ya Raia hasa Wananchi wanaonekana kuikosoa Serikali au wanaohoji matukio yasiyofaa kuhusu Viongozi wa Serikali ambapo Chama hicho kimeendelea kulaani vitendo hivyo.
Akiongea August 25,2024, Kiongozi wa ACT Wazalendo, Dorothy Semu amesema “Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kilitoa orodha ya Watu zaidi ya 89 waliopatwa na madhira hayo, Watanzania wameanza kuingiwa tena na hofu kukithiri kwa matukio haya.
“Inasikitisha zaidi kuona Watu wa kwanza wanaohusishwa na matukio haya ni Jeshi la Polisi na baadhi ya matukio Wananchi wanalalamikia Polisi kutochukua hatua za haraka kwa wanaohusika na matukio hayo”
“Chama cha ACT Wazalendo, tunalaani kwa nguvu zote kuongezeka kwa matukio hayo bila hatua madhubuti kuchukuliwa, ni wakati wa kusukuma madai ya mageuzi ya Jeshi la Polisi hasa kutoruhusu kutumika kisiasa, Jeshi la Polisi linapaswa kujiendesha kwa weledi”