Mlinzi bora wa Ligi Kuu msimu wa 2022/23 Dickson Job wa Klabu ya Yanga amerejeshwa katika kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kujiandaa na michezo miwili ya kufuzu ya Afcon 2025.
Mbali na Dickson Job pia yupo mlinda mlango wa Pamba Jiji ya Mwanza Yona Amos ambaye amekuwa na kiwango bora katika siku za hivi karibuni.
Tanzania ipo kundi H na itacheza mechi mbili za mwanzo dhidi ya Ethiopia na DR Congo.