Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.Hussein Ali Mwinyi amewaapisha Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali aliowateua hivi karibuni iliyofanyika Ikulu Zanzibar tarehe: 24 Agosti 2024.
Walioapishwa kuwa Makatibu Wakuu:
1.Dkt.Habiba Hassan Omar ameapishwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi .
2.Dkt.Mngereza Mzee Miraj ameapishwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya.
3.Ndugu Maryam Juma A.Saadalla ameapishwa kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais.
4 .Ndugu Khamis Suleiman Mwalim ameapishwa kuwa Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Kazi ,Uchumi na Uwekezaji .
Hafla hiyo ya uapisho imehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali , Dini na Vyombo vya ulinzi na Usalama.
#KonceptTvUpdates