Mbunge wa Kigamboni, Dkt. Faustine Ndugulile amechaguliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika baada ya kuwashinda wagombea wengine wanne wa nafasi hiyo kwenye uchaguzi uliofanyika leo Agosti 27, 2024 jijini Brazzaville nchini Congo.
Dkt. Ndugulile amewashinda wapinzani wake Dr Ibrahima Socé Fall (Senegali), Dkt. N’da Konan Michel Yao (Ivory Coast), Dr Richard Mihigo (Rwanda) na Dkt. Boureima Hama Sambo (Niger).
Kwa ushindi huo Dkt. Ndugulile anachukua nafasi inayoachwa na mtangulizi wake, Dkt. Matshidiso Rebecca Moeti raia wa Botswana ambaye amekamilisha uongozi wa vipindi viwili wa nafasi hiyo.