Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amesema mwezi Oktoba mwaka huu kutakuwa na maonesho ya magari yatakayovunja rekodi ya Guiness iliyowekwa na Ujerumani kwa kuwa na magari aina ya Land Rover 613 kwa wakati mmoja, ambapo kwa mkoa wa Arusha unaenda kuwa na magari aina ya Land Rover 1,000 kwa wakati mmoja.
“Rais tunakukaribisha mwezi wa kumi tarehe 12,13 na 14. Huu mji wetu Rais tunawaza hela tu yani hatuna mawazo mengine na tumekubaliana hata viongozi wa siasa, siasa tunayoifanya tuifanye ya pesa tu”,
“Tutakuwa na maonesho ya magari hayo na tunawaalika wananchi wote wa ndani na nje ya Tanzania kuja kuona vivutio vya utalii wa Arusha kupitia aina hii ya usafiri ya Land Rover”, amesema Makonda na kuongeza kuwa
“…Rais pia tunakushukuru sana kwa ajili ya Bilioni saba ya kupanua kiwanja chetu cha Kisongo, Arusha tunatumia uwanja wa Kilimanjaro na Kisongo. Hakuna mkoa wenye uwanja wenye miruko mingi kama Kisongo lakini tunaishia saa kumi na moja jioni ndege zinakuwa haziwezi kuruka tena”,
“Mkandarasi yupo site, tunafunga taa na kuna mita takribani 200-300 inaongezeka ili kuwa na run way ya takribani Km 2.1 ambayo itawezesha ndege yoyote kutua Arusha na kufanya shughuli za kiuchumi kuendelea kuwa kubwa zaidi.” amesema Makonda