Katibu wa NEC, itikadi na Uenezi CCM, Amos Makalla amethibitisha kupokea barua ya Jeshi la Polisi ya kukataa maombi ya kufanya mikutano ya hadhara Wilayani Ngorongoro na kubainisha kuwa Chama hicho kimeheshimu sababu za kukataliwa kufanya mikutano.
Hata hivyo Makalla amesema atafanya ziara Wilayani Longido, Karatu na Monduli baada ya kukataliwa kufanya mikutano Wilayani Ngorongoro.