Watu 70 sabini wamejeruhiwa baada ya mabehewa sita ya treni ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) kuacha njia ikitokea Kigoma kuja Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano TRC, Jamila Mbarouk amesema katika taarifa kwa umma kuwa hakuna kifo katika ajali hiyo na majeruhi wamekimbizwa katika hospitali ya Wilaya ya Uvinza kwa matibabu.
Kulikuwa na jumla ya abiria 571 na walioumia ni wanawake 26 na wanaume 44, amesema.