Rais wa klabu ya Nacional ya Uruguay, Alejandro Gaston Balbi Della Valle ametangaza kuwa familia ya mchezaji Juan Izquierdo ambaye amefariki siku kadhaa zilizopita, itapokea mshahara wa mchezaji huyo hadi mkataba wake utakapokamilika mwaka 2032.
Nacional itaendelea kulipa stahiki zote alizokuwa anatakiwa apewe mchezaji kama muajiriwa wa klabu hiyo, kuanzia mshahara mpaka Bonus kuanzia Sasa itapatiwa familia yake (mke na watoto wake)
Familia itapokea pesa kutoka kwenye mshahara wa aliyekuwa mchezaji wao Izquierdo,na mlengwa mkuu ni mke wake pamoja na watoto wake.
Juan Izquierdo amefariki dunia usiku wa kuamkia Agosti 28 akiwa na umri wa miaka 27 baada ya kukaa hospitali kwa siku tano akipatiwa matibabu baada ya baada ya kuanguka kwenye mechi ya Agosti 23 dhidi ya Sao Paulo katika hatua ya 16 bora ya Copa Libertadores.
Juan Izquierdo ameacha mke aitwae Selena, binti mwenye umri wa miaka miwili na mtoto mdogo ambayo hata mwezi bado hajafikisha.