Shirikisho la Soka nchini Nigeria limemteua mkufunzi raia wa Ujerumani, Bruno Labbadia kuwa kocha mkuu mpya wa Super Eagles.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 58 ambaye akiwahi kuwa kocha wa Bayer Leverkusen, Hamburg, VfB Stuttgart, VfL Wolfsburg na Hertha Berlin. Hii itakuwa kazi yake ya kwanza nje ya Ujerumani.
Changamoto ya kwanza ya Bruno itakuwa kutaja kikosi cha wachezaji 23 kwa ajili ya mechi zijazo za kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika.
Super Eagles wanatazamiwa kumenyana na Jamhuri ya Benin Septemba 7, na kufuatiwa na Rwanda siku tatu baadaye.