Chama cha Mapinduzi (CCM) kimetoa taarifa Septemba 1, 2024 kuwa Katibu Mkuu wake, Dkt. Emmanuel Nchimbi hakukimbia wala kudharau mdahalo uliopangwa kuwahusisha Makatibu Wakuu wa Vyama vya Siasa chini katika kituo cha Star Tv Agosti 31, 2024.
Taarifa hiyo imesema, Agosti 10, 2024 Mtangazaji Edwin Odemba alimtafuta Dkt. Nchimbi kwaajili ya kushiriki Mdahalo huo, alimueliekeza kuwasiliana na mratibu wa masuala hayo (Makalla) ambapo kwasababu anazozijua Odemba hakumtafuta.
“Kwa sababu ambazo Odemba anaweza kuzieleza mwenyewe, katika kipindi cha takriban wiki tatu, hakufanya mawasiliano au kumtafuta Ndugu Makalla kama alivyoelekezwa na kushauriwa na Katibu Mkuu Balozi Nchimbi”
“Tunaweza kutamka bayana na kwa uhakika kwamba Katibu Mkuu hakuwa ametoa uthibitisho wa kuhudhuria mdahalo huo. Hakukuwa na makubaliano yoyote rasmi ya yeye au mwakilishi wake kuhudhuria katika shughuli hiyo” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.
Aidha, CCM imesema kwa sasa Balozi Nchimbi yupo tayari kwa Mdahalo, Majadiliano na Makongamano yanayolenga maridhiano ya Kisiasa kadiri ya taratibu zilizopo na ratiba yake ya kazi inavyoruhusu.
It s a story of how your tax dollars are really spent and how disruptive ideas people are dealt with buy priligy paypal