Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amemuhamisha Abdallah Mussa Mwaipaya kutoka Wilaya ya Mwanga kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara akichukua nafasi ya Mwanahamisi Mukunda ambaye amehamishiwa kuwa DC wa Mwanga.
Rais amemuhamisha pia Victoria Charles Mwanziva kutoka Wilaya ya Ludewa kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Lindi ambapo nafasi yake inachukuliwa na Olivanues Paul Thomas ambaye ameteuliwa kuwa DC ya Ludewa, kabla ya uteuzi huu, Thomas alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Mafia.
Juma Issa Chikoka amehamishwa kutoka Wilaya ya Rorya kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Amir Mohamed Mkalipa amehamishwa kutoka Wilaya ya Hai kwenda kuwa Muu wa Wilaya ya Arumeru.
Na Halima Habib Okash amehamishwa kutoka Wilaya ya Bagamoyo kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chemba na Warda Abdallah Obathany amehamishwa kutoka Wilaya ya Iramba kwenda kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Kinondoni.
\
\