Watu wawili Iddi Mohammed na Janet Msigwa, wakazi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani Kigoma, wamekamatwa na kufikishwa Polisi na Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Kigoma kwa tuhuma za wizi wa maji ya bomba baada ya kuchepusha kwa muda mrefu bila kulipia bili za maji.
Iddi Mohammed mmiliki wa shamba la maua Goa Kigoma Ujiji, amemakatwa kwa tuhuma za wizi wa maji ambapo amekuwa akifungua mita na kufunga mlipa, kwa ajili ya kumwagilia shamba la maua la biashara, wakati Janet Msigwa mkazi wa Burega amefikishwa Polisi kwa kosa la kuunga mpira nyuma ya mita na kutumia maji hayo katika choo na bafu.
Chanzo; EATV